Wednesday, August 25, 2010

Usalama Waimarishwa

Kufuatia maandalizi ya sherehe ya kuidhinishwa kwa katiba mpya hali ya usalama jijini Nairobi imeimarishwa mara dufu haswa ikifahamika kuwa sherehe hiyo itahudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka nchi za nje.Idara ya polisi imesema hakuna yeyote atakayeruhusiwa kuingia katika bustani ya uhuru kuanzia kesho bila ya kupitia uchunguzi mkali kutoka kwa polisi na maafisa wa ujasusi.Ulinzi katika majengo yanayopakana na bustani hiyo ya uhuru vile vile umeimarishwa.

No comments:

Post a Comment