Saturday, July 24, 2010

Ndiyo Yaongoza


Mashirika ya Infortrack na Synovate yametoa utafiti wao mpya kuhusiana na matokeo ya kura ya maoni na katika tafiti zote mbili kura ya ndio imeorodheshwa kushinda katika zoezi la kura ya maoni. Shirika la utafiti la Infotrack limesema kuwa �ndiyo� ingeshinda kwa asilimia 65 ya wapiga kura huku asilimia 25 wakipiga �la� nalo shirika la Synovate limeorodhesha mrengo wa ndio kuibuka na ushindi kwa asilimia 58 huku mrengo wa la ukiwa na asilimia ya 27. Utafiti wao vile vile unaonyesha kuwa kati ya viongozi wa serikali walioko kwenye mrengo wa ndio, makamu wa Rais Kalonzo Musyoka ndiye wa mwisho kwa ushawishi ikiwa kwamba ni asilimia 49 pekee ya wafuasi wake wanaiunga mkono rasimu ya katiba. Anayeongoza ni Waziri Mkuu na asilimia 82, akifwatiwa na Rais Mwai Kibaki na asilimia 61.

No comments:

Post a Comment