Monday, August 16, 2010

Kurekebisha Katiba Mpya

Kamati ya wataalam iliwatahadharisha watu dhidi ya kuharakisha shughuli ya kuleta mabadiliko ya dharura ndani ya katiba na kuongeza kuwa hatua hii ya kuharakisha mabadiliko huenda ikatikisa msingi wa katiba mpya. Nzamba Kitonga mwenyekiti wa COE amesema ni muhimu watu kuwa na subira kwanza , lakini iwapo watasisitiza kuwepo kwa mabadiliko basi kuna njia za kisheria ambazo wanaweza kufuata kama kukusanya saini milioni moja na kadhalika, ingawa kwake yeye haoni haja ya mabadiliko ya dharura.

No comments:

Post a Comment